Msengenyaji ni mtu anayetoa taarifa za uongo na za kuharibu kuhusu mtu mwingine, kwa kawaida kwa lengo la kuharibu sifa ya mtu huyo. Usengenyaji mara nyingi huendeshwa na chuki na nia mbaya. Msengenyaji wa kazi ya Mungu na wa watumishi wa Mungu huwa na agenda ya kishetani ya kupunguza ushawishi na huduma ya mtumishi wa Mungu na pia kuharibu sifa ya Kanisa na watumishi wa Mungu. Katika enzi hii ya mitandao ya kijamii, usengenyaji umetumika kama silaha ya kuwaangamiza watu na kuchafua sifa zao walizojitahidi kuzijenga.
Katika kitabu hiki cha kufumbua macho, utajifunza mbinu za wasengenyaji na utapata faraja katika uhakika wa hukumu ya Mungu dhidi yao. Kwa mafundisho haya kutoka kwa Dag Heward-Mills, utainuka juu ya upinzani na kuwa mhudumu wa injili asiyezuilika!